By Wahu Kaara
Waceera dadangu ndugu kipenzi,
kipenzi shujaa mwenzangu
Shujaa Bintiye Mwalimu Kahiga,
kwa sifa sote tuijuaye
Sifa kijijini Ngorano tumeisikia,
Ngorano zawadi ya ulimwengu kote
Ulimwengu kote ukajulikana, Mama
Shujaa wa Kenya
Mama Shujaa Miriam Kahiga, Msomi
Mwandishi ukatambulikana kote
Uandishi usio na kifani, mawazo ya
kulenga na kuzinduwa
Wakenya wazalendo tukakujua,
heshima yako urithi wetu
Mama Shujaa Miriam Kahiga, Shujaa
mwenzangu kipenzi
Shujaa mwenzangu, mwenyezi
Mungu akamtambua
Yesu Kristo akawa nguzo yake,
ushuhuda ukatutolea
Ukaiishi imani yako, kwa matendo
na usemi
Injili ukaendeleza, na kuivumisha
mpaka hospitalini
Shujaa Mama mwenzangu, ukawalea
hata watoto
Uzazi ukauimarisha, wenye swali
waniulize
Madeni ya dunia umeyalipa, kwa
nini usifike Mbinguni
Waceera Mama Shujaa, historia yako
haifutiki
Tamati historia yako haifutiki,
maadili ya kifani umetuachia
Kuimarisha wema na utu, amri kuu
ya kupendana
Tabasamu yako nani usahau,
Waceera dadangu ndugu kipenzi
Waceera dadangu kipenzi, buriani
najua tutaonana







Please wait...











