Cheki!
Walituita tutokee
Tutokee referendum tupitishe katiba
Katiba ilikuwa lakini tukaambiwa hii ndio ile
Hii ndio ile katiba itahahakikishia mwananchi haki
Haki kwa wote na fundamentals
Fundamentals ziko kwa Bill of rights
But bill of rights, bill of rights imegeuzwa meal na knights
Knights wanasaka favours za kings
Kings wameji'brand vanguard
Vanguard ina'guard van kufikisha oppressor kwa safehouse
Safehouse haina room ya kulinda welfare ya victims
Victims wana'wish vitu zingekuwa safer
Safer juu wameletewa oppression na discount
Na discounts ziko lacking kwa bei za bidhaa
Bidhaa quality yake ni wanting
Wanting na sijaskia mention kwa idhaa
Idhaa za habari counterfeit
Counterfeit juu wanaleta propaganda kwa mitaa
Mitaa wakulima ni beggars
Beggars wamebeba nchi kwa bega... bega... bega
Bégá í mátúúró
Mátúúró jákámátíté máng’ótóré ná íkómbé
Íkómbé bíá nkíá bíkóójúríá bíóndó bíá ítóngá
Ítóngá bíkáríjáá íríó bía nkíá
Nkíá ígátígwá kúrúírá mátígárí
Mátígárí já wáthání
Wáthání bwájúkírwé kúrá ítítárí
Kúrá ítítárí ná cíátárwá bátítwáthá ná thíírí
Thíírí… thíírí
Thíírí ni amani
Amani haipatikani base mtaani
Mtaani mahali woolfer ziko on full volume
Full volume ndio zi'drown sauti za vilio
Vilio za wenyeji wana njaa
Njaa ni soundtrack na beats
Beats ni footsteps za raia kwa street Tom Mboya
Tom Mboya alidedi for a reason
Reason ilikuwa enough kwa mtu flani ku'commit treason
Treason zimekuwa committed lakini perpetrators bado hawajaona milango ya prison
Prison ni homestead kwa petty criminals na innocents alike
Na unlike maadili ya law school huku hela ndio inaamua nani ndio innocent na si innocent wallahi
Wallahi sijaielewa nini funny na jokes za hawa watu ma'times
Ma'times hizo jokes ni sisi zinakejeli na haifai
Haifai that najichunga na mtu bado ndiye anafaa kunichunga
Kunichinga haimanishi nikiuliza maswali ndio sasa unataka kunifunga
Kunifunga juu nimeuliza maswali yanadunga
Yanadunga sababu hauwezi eleza yaliendapi mahindi tulivuna
Mahindi tulivuna lakini watu wanakufa njaa juu hakuna unga
Hakuna unga na mavuno tulieka kwa store na tukafunga
Tukafunga na tukakupatia keys kama custodian
Custodian atwambie, amepataje pesa ya kununua keja Runda?
Umenunua nyumba Runda na mama mboga mtaani haezi fika bei ya unga
Bei ya unga ilipanda venye budget ilisomwa
Budget ilisomwa na waziri akasema, "Uchumi umepanda."
Uchumi umepanda kwa nani kama, "serikali saidia" ilishageuka national anthem
National anthem ni ombi
Ombi la nani kama raia Turkana wako fasting by force
By force nafaa kungoja kwa traffic ndio rais apite
Rais apite akapumzike kwa ikulu
Ikulu imejengwa mbali na mwananchi
Mwananchi anataka kuongea na rais but rais hafiki
Rais hafiki so inabidi ni nduru
Nduru kuu kwa wenye walipiga kura ndio rais apite... “Eeh… Rais apite! Rais apite!
Rais apite juu manifesto yake ilidai kupunguza bei
Bei za bidhaa zikipungua mwananchi anaeza afford ku'buy rice apike
Rice apike anga’ tumbo itakuwa na kitu akijipata kwa traffic akingoja rais apite
Rais apite lakini kwanza aseme nini ilifanyikia manifesto juu bado mwananchi haezi afford ku'buy rice apike
Rice apike ndio rais apite
Inakuwaje miaka nne baadae bado rice hapiki?
Rice hapiki na ata baada ya miaka nne ya nduru bado rais hafiki
Rais hafiki na ni mwaka mmoja, miwili, mitatu, mine…
eti na bado mwananchi anangoja...
Rais afike.
© Dorphanage 2018
By Ubax Abdi