Kupigwa na kupokonywa maisha
Hakutatuzuia sisi wananchi
Kunyakua Uhuru wetu
Na haki ya jasho letu
Jasho letu
Na haki ya jasho letu

Tumekataa kupiga magoti
Mbele ya hawa wauaji
Bila shaka sisi pia in watu
Hali ya utumwa tumeikataa
Katakata
Hali ya utumwa tumeikataa

Tutanyakua mashamba yetu
Tupiganie Uhuru wetu
Tuikomboe elimu yetu
Utamaduni na viwanda vyetu
Tukomboe
Utamaduni na viwanda vyetu

Sisi hatutaki kudhulumiwa
Hatutaki tena mauaji
Hili kupe tuliangushe
Haki na Uhuru zichanue
Zichanue
Haki na Uhuru zichanue

Uhuru wetu Wakenya Wakenya
Uhuru wetu Wakenya tupiganie
Mashamba yetu
Wakenya Wakenya
Mashamba yetu Wakenya
Tupiganie.

 

Leave a comment

Make sure you enter all the required information, indicated by an asterisk (*). HTML code is not allowed.